Blog Post

WAZIRI MHE KAPINGA ASHIRIKI MAJADILIANO YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA BANGOTE GROUP JIJINI LAGOS


Na Mwandishi wetu 

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Judith Kapinga[Mb],Agosti 07,2026,_  ameambatana na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Mipango na Uwekezaji, Mhe.Prof.Kitila Mkumbo(Mb) pamoja na Mawaziri wa sekta mbalimbali na Wakuu wa Taasisi za Serikali,katika Ziara ya kutembelea Viwanda na miradi mbalimbali ya Dangote Jijini Lagos,Nigeria.


Katika Ziara hiyo,ujumbe wa Serikali ya Tanzania umekutana na Uongozi wa Dangote Group na kujadili fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji nchini Tanzania,ikiwemo Mradi wa Bandari ya Bagamoyo na Kongani ya Viwanda,Uzalishaji wa Mbolea pamoja na uzalishaji wa Umeme kwa kutumia Makaa ya mawe.


Katika Ziara hiyo,Makamu wa Rais wa  Dangote Group, -DVG Edwin_ ametaka kufahamu mifumo na haki zinazopatikana kwa Wawekezaji nchini Tanzania,hususani katika  masuala ya Ardhi,Madini na uzalishaji wa Umeme.

Akijibu hoja hizo, Prof.Mkumbo amemuagiza Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu Tanzania (_TISEZA )pamoja na Wakuu wa Taasisi walioshiriki Ziara hiyo chini ya sekta husika na timu ya kiufundi,kukutana na Uongozi wa Dangote Group na kutoa ufafanuzi  wa kina kuhusu masuala hayo.


Hatua hiyo inalenga kuweka mazingira wezeshi kwa Wawekezaji  na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Dangote Group.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu