Blog Post

Makala

 

JINSI YA KUJENGA AFYA MTOTO KUANZIA MIEZI SITA


Kujenga afya ya mtoto kunahusisha mambo mengi kama chakula bora, malezi bora na mazingira mazuri ya kuishi.

Katika kipengele hiki ntazungumzia zaidi jinsi ya kujenga afya ya mtoto miezi sita na kuendelea kwa kuzingatia vyakula bora vyenye virutubisho muhimu.

Maziwa ya mama ni chakula bora na chanzo kikubwa cha lishe bora kwa mtoto kwani  maziwa ya mama ndani ya miezi sita ya mwanzo yanavirutubisho vyote muhimu vinavyohitajika kwa afya ya mtoto.

Mtoto tangu kuzaliwa anatakiwa kunyonya maziwa ya mama pekee bila hata kumpa maji hadi kipindi cha umri wa miezi sita anatakiwa kuanzishiwa chakula cha ziada kwani maziwa ya mama yanakuwa hayatoshelezi.

Katika kujenga afya ya mtoto tunatakiwa kuzingatia vyakula vyote vilivyo kwenye makundi matano ya chakula  kama protini, vitamini, wanga, madini na mafuta.

Vyakula kama matunda, mboga mboga, samaki, nyama, kuku, vyakula vya wanga kama nafaka, ndizi, viazi, mihogo pamoja vyakula jamii ya mikunde maharage, kunde, njugu mawe, choroko, soya nk.

Mtoto mwenye umri chini ya mwaka mmoja anayeanza kula chakula cha ziada tunashauriwa kumtengenezea lishe ya nafaka mchanganyiko usiozidi aina tatu na kuepuka kumpa lishe yenye mchanganyiko wa karanga.

Afya ya mtoto inatengemea sana malezi ya mama na familia kwa ujumla kwa mtoto anayeanza kula chakula cha ziada mama au mlezi wanatakiwa kumtia moyo wakati wa kula, kumuonesha mapenzi bila kumlazimisha kula, kumfokea au kumpiga.


Mazingira mazuri ya kuishi yanachangia sana kujenga afya ya mtoto, mazingira yasiyompa mtoto uhuru wa kucheza na wenzake hayamjengi kimwili, kiakiri kuimarisha misuli ya mwili wake na kumjenga kisaikolijia.



Post a Comment

0 Comments

Close Menu