Na Omary Mbaraka
Binti wa Rais wa Kenya, Mhe William Ruto, Charlene Ruto , amefanya sherehe ya jadi ya “Koito ak Chaik” lJumamosi, Agosti 8, 2026, katika eneo la Intona Heritage Farm, Kilgoris, Narok County , ikiwa ni sehemu ya mila za jamii ya Kalenjin kuelekea ndoa.
Kijana huyo ambae ni mfanyabiashara wa kitanzania mwenye umri wa miaka 36, anaitwa Isaya Yunge , ambaye ndie mchumba wa Charlene.Yunge pia ni mfanyabiashara na mtaalamu wa teknolojia kutoka Tanzania ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi Mtendaji wa SomaApps Technologies , kampuni iliyo nyuma ya SomaApp , jukwaa la kidijitali linalowaunganisha wanafunzi barani Afrika na fursa za elimu
Tukio hilo lilihudhuriwa na viongozi kadhaa wakubwa, akiwemo Naibu Rais wa Kenya Kithure Kindiki, Oburu Odinga, Mama Ida Odinga, Seneta Karen Nyamu na Mbunge Esther Passaris ..





0 Comments