Blog Post

MHE RIDHWANI KIKWETE ATEMBELEA JIMBO LAKE HUKU AKITATUA KERO ZA WANANCHI ILI MIRADI KADHAS KUKAMILIKA


 Na Mwandishi wetu


_Atoa fedha kukamilisha miradi ya afya na mabweni, aielekeza Ofisi ya Mkurugenzi kupeleka greda Talawanda, aendelee kutoa elimu tahadhari ya El nino._ 


Wiki hii, Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete alikua na ziara kabambe kwenye Kata 6 za Msata, Lugoba, Talawanda, Msoga, Ubena na Bwilingu ndani ya Jimbo kwa lengo la kuwashukuru wananchi kuendelea kuiamini CCM, kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuwezesha fedha iliyosimama pamoja na kufanya mikutano ya hadhara ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi.


Tarehe 16 ilikua zamu ya Kata ya Talawanda na Msoga. Akiwa Talawanda Sekondari, Mhe. Kikwete amekagua ujenzi wa vyoo kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum pamoja na hali ya mabweni ya wasichana akilenga kuhakikisha usalama na mazingira bora kwa wanafunzi shuleni hapo huku akiahidi kutoa milioni 80 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu na vyoo vingine matundu 10 kutokana na kutarajiwa ongezeko kubwa la wanafunzi shuleni hapo pamoja na milioni 30 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maabara shuleni hapo.


Aidha, Serikali ikiwa kwenye mpango wa kujenga mabweni ya wavulana shuleni hapo kwakua kwasasa kuna mabweni ya wasichana tu huku akielekeza kujengwa kwa uzio shuleni hapo kwa ulinzi zaidi.


Aidha ndani ya Talawanda hiyohiyo, Mhe. Kikwete amewahakikishia wananchi kwamba tayali milioni 30 imepitishwa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Kisanga huku akielekeza Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze inafika Kata ya Talawanda ili kuweka sawa miundombinu ya barabara.


Kwenye Kata ya Msoga, Mhe. Kikwete amekagua nyumba za watumishi wa afya kwenye Hospitali ya Wilaya ya Msoga na ujenzi wa zahanati Msoga huku kwenye mikutano yote na wananchi wa Talawanda na Msoga akisisitiza kuchukua tahadhari dhidi ya mvua kubwa za El nino zinazotarajiwa kutokea mwaka huu, viongozi kuimarisha utulivu, umoja na mshikamano ili kuchochea maendeleo.


Post a Comment

0 Comments

Close Menu