Na Mwandishi wetu
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Salvio Kapinga (Mb.), amekutana na Meneja Mkuu wa Haofeng Group Company, Ahmed Hashim Ngahemela (Petitma), pamoja na Meneja Mauzo wa kampuni hiyo, Jordan Jubicate Uroki, kujadili mpango wa kuanzisha kiwanda cha kuunganisha magari yanayotumia nishati ya umeme nchini.
Katika mazungumzo hayo, Waziri Kapinga na viongozi hao wamejadili fursa na hatua zinazohitajika katika kutekeleza mpango huo, ambao unalenga kuongeza uwekezaji na uzalishaji wa ndani katika sekta ya magari.
Uanzishwaji wa kiwanda hicho unatarajiwa kuchangia katika uendelezaji wa teknolojia ya magari yanayotumia nishati ya umeme, kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania na kukuza mnyororo wa thamani katika sekta ya magari nchini.




0 Comments