Na Omary Mbaraka
Waziri wa utumishi na utawala Bora ofisi ya Rais Mhe Ridhwani Jakaya Kikwete ashiriki kilele cha Sherehe ya Miaka 25 ya Chuo Cha Utumishi Wa Umma Tanzania kilochofanyika katika Ukumbi wa JNICC-Dar Es Salaam.
Katika sherehe hizo ambazo zimepambwa na Mwaliko wa Wakuu waliopita wa Chuo hicho an Taasisi ambazo Zimefanya kazi na Chuo hicho katika kipindi cha miaka 25, alipokea na kutoa vyeti na tunzo za shukrani kwa wote walioshiriki kufikia mafanikio ya Chuo hicho jana. Katika sherehe hizo pia, aliwakumbusha umuhimu wa chuo hicho kwa Watanzania hasa umuhimu wa kuendelea kufundisha na kukuza utumishi wa Umma Tanzania.





0 Comments