Na Omary Mbaraka
Mkutano huo ambao umewakutanisha maafisa Tawala na Rasilimali Watu toka Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, Zile zinazojitegemea na Zile za Serikali ya Mitaa umefanyika ikiwa ni Mkutano wa Mwaka unaokutanisha wataalamu hao ambapo wanajadili mambo mbalimbali yanayohusu changamoto za fani yao na jinsi ya kukabiliana nazo. Mkutano huu wa Mwaka umeandaliwa na Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora na ni mkutano ambao umuhimu wake unawezesha serikali kukutana na wataalamu ikiwa ni mpango wa kuboresha utumishi wa Umma.
Katika mkutano huo, Mhe Kikwete amewakumbusha kufuata taratibu na kuimarisha mawasiliano baina ya ofisi zao na ofisi ya Rais- Utumishi ili kuimarisha utatuzi wa changamoto huku msisitizo mkubwa akisisitiza kuweka kwenye matumizi ya teknolojia za mawasiliano yaani mifumo iliyowekwa na kutengenezwa na Serikali kupitia Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora. Pia Mhe Kikwete alitumia nafasi hiyo kumshukuru Mh. Rais kwa kazi kubwa na maelekezo anayoyatoa yanayofanikisha utendaji kazi wao na kuimarisha huduma kwa wananchi huku akigusia mafanikio makubwa ya ujenzi wa mifumo, upandishaji madaraja,ulipwaji wa madeni yanayotokana na mishahara na likizo.
#KaziNa Utu #TunasongaMbele #KaziInaendelea







0 Comments