Blog Post

MMILIKI WA HOSPITALI KISUTU MATATANI


Na: Anania Njonjo

Mfanyabiashara mmoja mwenye asili ya Kiasia (Mhindi) jina kapuni, anayemiliki hospitali moja katika Kata ya Kisutu, analalamikiwa na Wafanyakazi wake kwa manyanyaso mbalimbali.

Kutokana na manyanyaso hayo, ikiwa ni pamoja na kutopewa Mikataba, kutopeleka mafao yao kwenye Mifuko ya fedha ya Kijamii ya NSSF, WCF, nk. lakini pia kutopewa likizo na mbaya zaidi kwa kutotoa risiti za EFD kwa wagonjwa, wameamua kutafuta chombo hiki cha habari kiwasemehe.

Baada ya kupokea malalamiko hayo, Waandishi wa chombo hiki cha Tafakari News Weblog, walimfuata Mkurugenzi Mkuu (Mwenye hospitali) na kuhojiana naye (Interview) ambaye alikiri na kuomba kurekebisha kasoro hizo mwishoni mwa mwezi huu wa July 2026   “Ni kweli ila nimeshaongea na Wafanyakazi wangu, nimewahakikishia marekebisho yote mwisho wa mwezi huu wa saba, alisema”.

Chombo hiki kinajiuliza je huu ni utaratibu wa ajira? Isitoshe, hii ni hospitali ya muda mrefu, iwapo kwa muda wote huu alikuwa akiwepa kodi (receipt) ameshajinufaisha kwa kiasi gani? 

Haya, mwisho wa mwezi huu wa saba (July 2026), Waandishi hao waliahidi kufuatilia marekebisho hayo ili Wafanyakazi wapate haki zao pia kwenda TRA kujua hatia watakazo chukua. Hata hivyo, Mwajiri huyo alipoambiwa na Waandishi sababu za kufanya hayo, aliwatisha kwa kumpigia simu Mwenyekiti wa Mtaa huo ajulikanaye kwa jina la Bwana Daluga akiamini wangeogopa lakini haikuwa hivyo, ndipo Mwenyekiti alikubaliana kwa kuandikwa ili iwe onyo kwa wengine katika Mtaa wake akidai hakuwa na habari ya Hospitali hiyo kufanya hayo. “Sina taarifa hiyo ila andikeni kwani mtakuza jina lake, alijibu kwa kifupi Mwenyekiti huyo.” 

Toleo lijalo tutawatajia jina la Hospitali na Mmiliki wake baada ya kupata majibu toka TRA na Idara ya Kazi (Labour) kwa hatua alitakazochukuliwa.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu