Blog Post

SERIKALI ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WAWEKEZAJI WAZAWA -KAPINGA


Na Omary Mbaraka 


Jijini Dodoma_

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Judith Kapinga[Mb]_ amesema Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan_ itaendelea kushirikiana na Wawekezaji wazawa kwa kuondoa vikwazo vinavyoweza kudhoofisha jitihada zao za kuwekeza na kukuza Uchumi wa Nchi.

Kapinga_ amesema hatua hiyo inaendana na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayolenga kujenga uchumi wa Viwanda unaotegemea zaidi uwekezaji wa ndani na ubunifu wa Watanzania.


Waziri Kapinga_ ameyasema hayo,  juni 24,2025_wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Mafunzo,Ufundi na Utengenezaji wa Magari cha Superdoll jijini Dodoma.Kituo hicho kimezinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Mwigulu Nchemba.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu