Blog Post

BARUA KWA WAZIRI MKUU TATIZO LA ARDHI DODOMA

 Na Mwandishi wetu

Wananchi wa eneo la mbwanga jijini Dodoma wamejikuta Katika mgogoro mkubwa wa ardhi na baadhi ya nyumba zao kubomolewa na hata hivyo juhudi zao kuomba utatuzi toka idara ya ardhi kushindikana sasa wameamua kufikisha ujumbe kwa waziri mkuu kama ifuatavyo; 


Mheshimiwa Waziri Mkuu,


Sisi ni Wakazi wa Mbwanga-Dodoma jiji.

Kwa unyenyekevu na heshima kubwa tunakuomba uingilie kati mgogoro wa ardhi unaoendelea  Mbwanga–Mtagamalee jijini Dodoma* .


Wakazi halali tulipimwa na kutambuliwa mwaka 2018, lakini  Bw. Abdallah Nyakongo, akisaidiwa na baadhi ya WATUMISHI  WASIO WAAMINIFU WA IDARA YA ARDHI JIJINI, anadai umiliki bila ushahidi na amebomoa baadhi ya nyumba zetu.


Malalamiko yetu kwa mamlaka mbalimbali ikiwemo serikali ya mkoa na wialaya hayajasikilizwa. 


Tunaomba hatua za haraka, pamoja na uchunguzi wa kina hasa *FORENSIC VERIFICATION* ya Nyaraka zote alizopatiwa Bw. Nyakongo, ili kulinda haki za wananchi na kudumisha imani kwa serikali yetu tukufu chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hata baada ya Mwandishi wetu kuongea na baadhi ya wananchi Dodoma inaonekana mkoani Dodoma Kuna maeneo mengi yana migogoro kama vile Ndachi nk lakini utatuzi wake ni WA kusuasua.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu