Na Omary Mbaraka
RAIS wa Kenya Dkt William Samoei Ruto Leo hii tarehe 5 may 2026 amehitimisha ziata yake kwa kuhutubia BUNGE LA Tanzania.
Ambapo alianza kwa kusema "Kiswahili kilizaliwa Zanzibar kikaja Tanzania bara kikakua na kubalehe kikaenda Kenya kikaugua kikaenda Congo huko kikafa"
MHE Ruto pia alisema Tanzania na Kenya sio maadui ila tunao maadui nchini mwetu na Tanzania nao wanaitwa"Kukosa ajira na Umasikini hivyo amemba nchi hizi mbili zishirikiane na KUWEKA miundo mbinu ili kukuza biashara Katika nchi hizi mbili
Pia alifurahi na kuyataja makampuni yaliowekeza Kenya kutoka Tanzania nayo ni Taifa gas, lake gas na Amson group ambapo alisema Kenya wamewekeza Tanzania USD 1.7 Bilioni na Tanzania imewekeza Kenya USD milioni 300
Mhe Ruto pia alisema siku Moja walizungumza na Rais Museven wa Uganda na kumshauri kwanini mafuta uchimbe Uganda na kuyapeleka nje kuyasafisha si Bora ungejenga "Refinery" hapo Uganda akamjibu hana uwezo hivyo akamshauri nchi tatu za Afrika Mashariki ziungane na kujenga Refinery wakakubaliana hivyo MIKAKATI unapangwa ili kujenga Refinery hio ambayo mbali na kujitegemea kwa mafuta pia yatauzwa kwa bei nafuu



0 Comments