Waziri Mhe Paul Makonda wa Wizara ya Habari na utamaduni leo hii amewakilisha maombi ya bajeti ya T shs bilioni 525.3 akiweka vipa umbele vya matayarisho mashindano ya AFCON yatakayofanyika mwaka 2027,,maandalizi ya miss world, gharama za mishahara na kuwapa mtaji watoa maudhui kuongeza ajira kwa vijana.
Aidha, Mheshimiwa Makonda alisema Serikali kupitia JAB imeandaa mwongozo maalumu wa kisheria utakaowawezesha Waandishi wa Habari wakongwe walioathiriwa na mfumo wa ithibati kureiea katika mfumo rasmi, kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229 ambayo ilitungwa kwa ajili ya kukuza taaluma ya uandishi wa habari.
Mwandishi wa Habari hizi anampongeza sana MHE Makonda kuwarejesha waandishi wa Habari wakongwe kurejea Katika mfumo kwani tumeshuhudia kuwa kigezo cha uzoefu wa muda mrefu ni muhimu hata Katika fani mbali mbali kwani tumewahi kushuhudia mafundi wa magari wazoefu wa miembeni kuwa mahodari na wateja wengi kuwakimbilia kuliko fundi aliesoma Chuo cha ufundi lakini ana uzoefu wa muda mfupi vivyo hivyo hata Katika uandishi wa Habari.





0 Comments