Blog Post

RAIS MSTAAFU DKT JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA MSHAURI WA TRUMP NORWAY


 Na Mwandishi wetu 

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanya mazungumzo na Bw. Massad Boulos, Mwanadiplomasia na Mshauri Mwandamizi wa Rais wa Marekani, Donald Trump anayeshughulikia masuala ya Nchi za Afrika, Uarabu na Mashariki ya Kati.


Mazungumzo hayo yamefanyika pembezoni mwa Mkutano wa Oslo Forum 2026  jijini Oslo, Norway, kuanzia  Juni 10 hadi 12, 2026.


Mkutano huo umewakutanisha Viongozi, Wanadiplomasia Waandamizi na Wataalamu wa masuala ya amani na usuluhishi kutoka Nchi mbalimbali duniani kwa lengo la kujadili changamoto za usalama, diplomasia na juhudi za kuimarisha amani katika maeneo mbalimbali ya dunia.


Post a Comment

0 Comments

Close Menu