Blog Post

MAJIKO BUNIFU KUWAOKOA WANANCHI

 Na Mwandishi wetu 


Wakala wa nishati vijijini REA wamedhamiria kuhakikisha azma ya serikali inatimia ya kuwawezesha wananchi zaidi ya asilimia themanini wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034


Mhandisi Deusdedit Malulu  ( KOMANYA )  mhandisi kutoka wakala wa nishati vijijini REA akiwa jijini Mwanza amesema mradi wa majiko bunifu ambayo yanatumia mkaa na kuni kidogo yatasaidia kuifikia azma hiyo ili wananchi wake watumie nishati safi itakayosaidia pia kutunza mazingira


Mhandisi Malulu amesema kwa mkoa wa Mwanza wametenga zaidi ya milioni mia nne kwa ajili ya kuhakikisha wakazi wake hasa waishio vijijini wanapata majiko hayo bunifu ambapo kwa awamu ya kwanza majiko elfu kumi na mbili yatatolewa


Aidha mhandisi Malulu amesema wananchi watalipia shilingi elfu saba na mia tano huku asilimia nyingine ikilipwa na serikali kupitia REA


Mkuu wa mkoa wa Mwanza Said Mtanda akipokea majiko hayo sanifu amewapongeza REA kwa kubuni mradi huo ambao utawawazesha wananchi kutumia nishati safi na kwa bei nafuu huku akiwashauri REA kuyaboresha zaidi majiko hayo ili yatumike kwenye shughuli mbalimbali za wananchi


Kwa upande Salma Sudy ambae ni afisa masoko kutoka kampuni ya Envotec services limited ya kutengeneza majiko banifu na sanifu aina ya majiko makini yanayotumia nishaiti safi ya kupikia amesema wamashirikiana na wakala wa nishati vijijini REA kwa ajili ya kutengeneza majiko hayo ili kuhakikisha wananchi wanatumia nishati safi



Post a Comment

0 Comments

Close Menu