Blog Post

MHE MCHENGERWA-TEKNOLOJIA NA YA VIJANA YANGARA TANZANIAA




Na John Mapepele, New York – Marekani 


Serikali ya Tanzania imeweka wazi mkakati wake wa kutumia teknolojia na nguvu ya idadi kubwa ya vijana kama nyenzo kuu ya kuharakisha maendeleo endelevu, ikisisitiza umuhimu wa utafiti na ubunifu ili kukabiliana na changamoto za kijamii na kiuchumi.


Akihutubia Mkutano wa 59 wa Idadi ya Watu na Maendeleo unaofanyika New York kuanzia Aprili 13 hadi 17, 2026, Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema kuwa Tanzania inaendelea kuimarisha sera na mikakati itakayohakikisha mapinduzi ya teknolojia yanawanufaisha wananchi wote bila ubaguzi.


Amebainisha kuwa matumizi sahihi ya teknolojia yana uwezo mkubwa wa kubadilisha mwelekeo wa maendeleo, huku akisisitiza kuwa serikali inaunga mkono juhudi za kimataifa zinazolenga kuunganisha teknolojia, tafiti na maendeleo ya watu.


Katika hotuba yake, Mchengerwa ameweka mkazo kwenye nguvu ya vijana, akieleza kuwa Tanzania ina idadi kubwa ya vijana ambao ni rasilimali muhimu ya kukuza uchumi jumuishi na endelevu huku akisisitiza kuwa uwekezaji katika elimu, ujuzi na ajira kwa vijana ni hatua muhimu ya kuleta mageuzi ya kiuchumi.


Aidha, amefafanua kuwa masuala ya idadi ya watu yamepewa kipaumbele kwenye mipango ya maendeleo ya taifa, ikiwemo Dira ya Maendeleo ya 2050 na Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano, yote yakilenga kuendana na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).


Katika sekta ya teknolojia, Tanzania imepiga hatua kubwa kupitia uwekezaji wa miundombinu ya kidijitali, hususan Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na Mradi wa Tanzania ya Kidijitali, hatua iliyoongeza upatikanaji wa huduma za serikali mtandao na kuimarisha ujuzi wa kidijitali, hasa katika maeneo ya vijijini.


Mchengerwa pia amesisitiza umuhimu wa takwimu sahihi katika kupanga maendeleo, akitaja mafanikio ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 pamoja na maboresho ya mfumo wa usajili wa vizazi na vifo (CRVS).


"Katika sekta ya afya, serikali inaendelea kutekeleza huduma ya afya kwa wote kupitia Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote ya mwaka 2023, huku matumizi ya teknolojia kama tiba kwa njia ya mtandao yakiboresha utoaji

Post a Comment

0 Comments

Close Menu