Blog Post

DKT JAKAYA M KIKWETE NI MWAKILISHI MAALUM WA PEMBE YA AFRIKA NA BAHARI YA SHAMU


 Na Omary Mbaraka 

Rais mstaafu Mheshimiwa  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameaminiwa na African Union (AU) na kuteuliwa kuwa Mwakilishi Maalum wa Pembe ya Afrika na Bahari ya Shamu. Hii ni heshima kubwa si kwake tu, bali pia kwa Tanzania na Bara zima la Afrika. 


Kwani ni ukweli hivi sasa Afrika inahitaji sana sauti ya hekima na juhudi za dhati katika kujenga amani, hivyo uteuzi wake unaonesha imani kubwa iliyowekwa juu yake katika kusimamia diplomasia ya kuzuia migogoro, kuimarisha mazungumzo jumuishi ya kisiasa na kujenga uaminifu miongoni mwa wadau mbalimbali. 


Hakika, uwezo wake wa kutafuta suluhisho bunifu na endelevu ndio msingi hasa katika kipindi hiki ambacho Afrika inahitaji sana sauti ya hekima na juhudi za dhati katika kujenga amani, uteuzi wake unaonesha imani kubwa iliyowekwa juu yake katika kusimamia diplomasia ya kuzuia migogoro, kuimarisha mazungumzo jumuishi ya kisiasa na kujenga uaminifu miongoni mwa wadau mbalimbali. 


Uteuzi huu ni ushahidi wa wazi wa hazina yake adhimu ya uongozi, uzoefu mpana wa kidiplomasia, pamoja na uadilifu na busara alizoendelea kuzionesha kwa miaka mingi katika ngazi za kitaifa, kikanda na kimataifa. Ameendelea kuwa kielelezo cha kiongozi mwenye maono, utulivu wa fikra na uwezo wa kuunganisha watu kwa ajili ya pamoja


Aidha, tunatambua na kuthamini umahiri wake wa kuratibu wadau wa kimataifa na kikanda wakiwemo "Intergovernmental Authority on Development, East African Community, League of Arab States" pamoja na United Nations katika kuleta mshikamano, ufanisi na mwelekeo mmoja wa juhudi za kulinda amani na usalama wa kikanda. 

Taasisi hii ya habari inamuombea afya njema, MHE Kikwete na hekima zaidi na nguvu ya kuendelea kukabiliana na changamoto zilizopo, huku akisukuma mbele ajenda ya amani ya kudumu, ustawi na maendeleo ya Bara letu.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu