Blog Post

SERIKALI KUENDELEA KULINDA UHURU WA KUABUDU -RAIS SAMIA

 Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kulinda uhuru wa kila Mtanzania kuabudu kulingana na imani yake, huku akisisitiza umuhimu wa kuheshimu mipaka ya uhuru huo ili kudumisha amani na mshikamano wa taifa.


Ameyasema hayo leo Jumamosi, Machi 21, 2026 wakati akishiriki Baraza la Idd El-Fitr 

Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Samia amesema Serikali inatambua na kuheshimu haki ya msingi ya uhuru wa kuabudu, lakini akaonya kuwa uhuru huo unapaswa kutumika kwa kuwajibika. jijini Dar es Salaam.“

"Nataka niwahakikishie kuwa serikali yetu itaendelea kutimiza wajibu wake wa kikatiba wa kulinda uhuru wa kila Mtanzania kuabudu kulingana na imani yake. Pamoja na hayo, ni muhimu kwetu sote kuheshimu mipaka ya uhuru huo,” amesema.

Ameongeza kuwa: “Hatuna budi kuheshimu sheria za nchi na haki za wengine ili uhuru huo usigeuke kuwa chanzo cha chuki, mgawanyiko au kuvuruga amani na mshikamano wa taifa letu.”
Amekemea suala la matumizi ya akili mnemba kutumika vibaya kuwatukana viongozi wa serikali na wa dini huku akisema Watoto wakiona mambo hayo nchi haitakuwa salam.
“Hatuna budi kuheshimu sheria za nchi na haki za wengine ili uhuru huo usigeuke kuwa chanzo cha chuki, mgawanyiko au kuvuruga amani na mshikamano wa taifa letu,” amesisitiza Rais Samia.Aidha, 

Rais Samia ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuenzi umoja, mshikamano na kuvumiliana kidini, akibainisha kuwa misingi hiyo ndiyo nguzo muhimu ya kudumisha amani na “Nchi haitatulia maendeleo hayatakuwapoi kwa sababu kutakuwa na vurugu, viongozi wa dini endeleeni na jukumu hili muhimu kuwajenga wananchi na kuwaelekeza ili tuwe na taifa lenye amani, utulivu, ustahamilivu ili tuwe na kizazi bora cha sasa na kijacho,” amesema. wa nchi.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu