Blog Post

KAMATI YA BUNGE YA UWEKEZAJI MITAJI (PIC) YATEMBELEA MRADI WA DART



Na Omary Mbaraka 


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Masanja Kadogosa, tarehe 23 Machi, 2026 imetembelea na kufanya ukaguzi wa mradi wa Miundombinu ya Mabasi yaendayo Haraka (DART) Jijini Dar es Salaam.


Kamati hiyo ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imepokelewa na Menejimenti ya DART pamoja na TANROADS na kufanya ziara ya Ukaguzi wa mradi huo wa awamu ya tatu (Posta Mpya - Gongo lamboto) ambapo Serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwa lengo la kutoa huduma bora ya usafiri kwa Watanzania.


Aidha, Kamati hiyo imetoa maelekezo kwa Waziri wa Ujenzi kumsimamia kikamilifu Mkandarasi wa mradi huo ili aweze kumaliza kwa wakati, DART kuandaa mpango kazi wa kukarabati vituo vya Mwendokasi pamoja na kushirikiana na taasisi muhimu kwenye mipango ya ujenzi kama vile TANESCO, DAWASA, TPDC.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu