Blog Post

KIKWETE AKABIDHI VIFAA TIBA,GARI LA WAGONJWA NA GARI LA ZIMAMOTO JIMBONI

 Na Omary Mbaraka 


Kipaumbele cha kwanza Chalinze ni uboreshaji wa huduma za kijamii kwa wananchi na Jimbo la Chalinze limeendelea kupata maendeleo makubwa kwa kushuhudia uzinduzi wa miradi mikubwa ya maendeleo.


Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amefanya ziara jimboni kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa pamoja na kupokea gari la Zimamoto na gari la kubebea wagonjwa (Ambulance).


Kwenye ziara hiyo, Kikwete amekagua mradi wa kituo cha afya Kata ya Vigwaza ambapo amekabidhi vifaa tiba na kutoa ruhusa ya kuanza huduma, maendeleo ya Ujenzi wa Zahanati Kijiji cha Ruvu Darajani, Kijiji Cha Pera, Ujenzi wa Madarasa Sita Shule ya Chalinze, kupokea Gari la Zimamoto na Gari la Wagonjwa -Zimamoto Chalinze na kumalizia na Ujenzi wa Mabweni ya Wanafunzi Shule ya Sekondari ya Chalinze.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu