Na Omary Mbaraka
MFANYABIASHARA Ally Khalfan Rubeya amewaonya wahuska wa familia ya Ernest Mashimba, kuacha kuendeleza chokochoko kwa kuwa wameshindwa katika mihimili yote ikiwemo mahakama
Mbali na onyo hilo, ametahadharisha anaweza kuanza kuchukua hatua dhidi yao na hasa Rose Mashimba ambaye ni mjane wa Mashimba.
Hayo yamebainishwa na wakili wa kujitegemea Steven Mosha ambaye anamwakilisha mfanyabiashara Rubeya.
Mosha alisema madai yote yaliyotolewa na Rose kwa nyakati tofauti na kwa mamlaka mbalimbali yalimpa ushindi mteja wake katika. Chanzo cha sakata hilo ambalo ni kiwanja namba 9, Ursunol Estate, Dar es Salaam.
Alisema hapo awali, Rose aliingia kwenye mahusiano ya kibiashara na Rubeya kuhusiana na kiwanja hicho ikiwemo kupewa nyumba mbili zilizotolewa eneo la Magomeni na viwanja viwili vilivyotolewa Mbweni jijini Dar es salaam na bw Rubeya
Vitu hivyo vikijumuishwa na gari aina ya Toyota Prado vina thamani ya Sh. milioni 800. Vikiwa ni sawa na thamani ya plot namba 9, Ursunol, Dar es Salaam.
“Masharti yalitekelezwa na makubaliano yote kufikiwa kisheria, lakini Rose kila mara amekuwa akiibuka na kuzusha madai tofauti, sasa tunamtaka aache,”alisema Mosha.
Kutokana na kauli mbili tofauti zilizotolewa hivi karibuni na waziri wa Ardhi na naibu waziri wa Ardhi ambazo kifupi zilitoa msisitizo na onyo kuwataka maafisa Ardhi wasiwe sehemu ya mgogoro na wakifahamika watasimamishwa kazi..Hivyo upande wa Rubeya umeamua kuchunguza na wakibaini maafisa Ardhi wanaohusika wataripotiwa kwa Waziri



0 Comments