Na Omary Mbaraka
Jengo la gorofa mbili linalojengwa maeneo ya ubungo kibangu linalomilikiwa na bw Denisi Mrema limesababisha kifo Cha mwanafunzi wa chuo Cha maji ajulikanae Juma ama jina la utani Ngosha
Jengo Hilo lilikuwa likijengwa bila kufuata taratibu na sheria husika kwani halikusajiriwa na bodi husika za CRB, ERB na hivyo halikuwa na bango kuonyesha usajiri huo kwani lilikuwa likijengwa na mafundi wa mitaani ambao pia hawakuzingatia taratibu husika kama kuvaa vitendea kazi wakati wa UJENZI kama kofia ngumu ( helmet), gloves nk
Tarehe 8 February 2026 marehemu Juma ama Ngosha alilazimika kwenda katika jengo Hilo kuomba kibarua ili aweze kulipa ada ya chuoni hapo ingawaje hana ujuzi wa ujenzi na kwa vile jengo lenyewe lilikuwa likijengwa bila utaalamu husika alipewa kazi ya kibarua Cha kuchanganya zege juu ya gorofa ya pili na hivyo kwa vile hakuna vitendea kazi hakuvaa kofia ngumu ambayo ingemsaidia asiumie kichwani kwani inasemekana maumivu makubwa na damu nyingi kutoka kichwani. Marehemu baada ya kuanguka mida ya saa sita alikimbizwa hospitali ya mwananyamala na kufatiki saa kumi
Suala hili liliripotiwa polisi ambao hivi Sasa jengo Hilo limezungushiwa utepe kusifanyike cho chote




0 Comments