Blog Post

MBUNGE MHE SAMIRA KHALFAN AMOUR(MZUNGU) ATUNUKIWA HATI YA HESHIMA


 Na Mwandishi wetu 


Jumuiya ya Umoja Wa wanawake Tanzania Chini ya Mwenyekiti wake Wa UWT Taifa Ndugu MCC Mary Pius Chatanda (Mb) imemtunuku hati ya  Pongezi na Shukrani Mbunge Wa Viti maalum kutoka Mkoa Wa Kagera  Mhe Samira Khalfan Amour (Mzungu) kwa Mchango wake, juhudi, weledi na uzalendo Wa kipekee aliouonesha katika Uchaguzi Mkuu 2025 uliopelekea ushindi Wa kishindo kwa Chama cha Mapinduzi (CCM).


Baada ya kupokea hati hiyo Mbunge Mhe Samira Khalfan Amour (Mzungu) `ameandika`;


"Nichukue nafasi hii kuwashukuru Sana viongozi wangu wa UWT ngazi yaTaifa kwa kutambua,  kuthamini na kuniteua katika hatua ya awali kuwa Mjumbe Wa Kamati ya kusaka ushindi Wa CCM katika Uchaguzi Mkuu 2025.  


Kipekee ninawashukuru sana wanawake wote na Jumuiya nzima ya UWT Mkoa wa kagera kwa ushirikiano mlionipatia binti yenu na Cheti hiki cha Pongezi na Shukrani nimekipokea kwa niaba yenu mama zangu wote wa kagera."



Post a Comment

0 Comments

Close Menu