Na Mwandishi wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameteuliwa rasmi kuwa Kinara wa Umoja wa Afrika (AU) wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto (Maternal, Child and Reproductive Health).
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari S. Machumu, uteuzi huo umeidhinishwa katika Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU uliofanyika tarehe 14 Februari 2026, jijini Addis Ababa, kufuatia mapendekezo ya Ripoti ya mwaka 2025 ya Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu Africa Centres for Disease Control and Prevention
Machumu amesema kuwa katika wadhifa huo wa mwaka mmoja, Rais Dkt. Samia ataongoza juhudi za kuimarisha mshikamano na hatua za pamoja miongoni mwa nchi wanachama wa AU katika kuboresha afya ya uzazi pamoja na afya ya mama na mtoto barani Afrika. (Africa CDC).




0 Comments