Na Ismail Mang'ola
MWEKEZAJI wa kigeni hapa nchini ambaye ni raia wa Pakstan amekuwa akifuatiliwa na Idara mbalimbali za Serikali.
Mwekezaji huyo aliyefahamika kwa jina moja la Zubair anayemiliki Mgahawa unaojulikana kwa jina la Karachual Restaurant ulipo mtaa wa Chaga Ilala jijini Dar es Salaam.
Chanzo chetu Cha habari kimebainisha kwamba Mwekezaji huyo amekuwa akifuatiliwa na Idara mbalimbali za Serikali kitu ambacho kinatia mashaka katika uwepo wake pamoja na uwekezaji aliouomba.
Baadhi ya vyanzo vyetu vimeendelea kudai kuwa, raia huyo amekuwa akifuatiliwa na Idara ya Uhamiaji, Manispaa pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA.
Mbali na Idara hizo kufatilia mwenendo wa Mwekezaji huyo, pia chombo hiki kilipeleka timu ya waandishi wa habari kwa ajili ya kupata ukweli juu ya taarifa hizo na kufanikiwa kuonana na mtu aliyejitambulisha kwa jina moja la Dorece na alipoulizwa baadhi ya maswali alikiri lakini akasema mzungumzaji zaidi ni Mwanasheria wa Kampuni.
Juhudi za kumpata mwanasheria zilifanikiwa lakini pia alisema jambo Hilo lipo chini ya mtoto wa Mkurugenzi aliyetambulika kwa jina la Anas na alapopigiwa simu ya kiganjani hakupokea
Habari hizo zinaendelea kudai kwamba,TIN na Lesni zilizokuwa zikitumika hapo awali zilikuwa sio za Kampuni ya mwekezaji huyo zilikuwa za Dorece ambaye ni mfanyakszi wake
Mbali na Mgahawa huo, vyanzo vyetu viliendelea kubainisha kuwa, awali mwekezaji huyo wakati anaomba kibali, aliomba kibali Cha kufungua Kampuni inayoitwa Hinopack Tanzania Limited ambayo alitaja kuwa na uwekezaji mkubwa ili afanikiwe kupata vibali husika
Kwakuwa chombo hiki Bado kinaendelea kufatilia kwenye Idara hizo za Serikali ili kujua ukweli na baada ukweli huo tutaweka wazi kwenye toleo letu lijalo



0 Comments