Blog Post

MHE KAPINGA AZITAKA SEKTA ZA UZALISHAJI KUZALISHA BI BIDHAA ZA MWISHO ZENYE UBORA


Na Mwandishi wetu

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Judith Kapinga[Mb] amesisitiza kuwa manufaa makubwa ya rasilimali zilizopo nchini yatapatikana Tanzania itakapowekeza katika kuchakata na kuzalisha bidhaa za mwisho zenye ubora wa juu badala ya kuuza malighafi ghafi nje ya nchi. 


Mhe Kapinga ameyasema hayo  Julai 06,2026 akizungumza katika maadhimisho ya Jubilei ya Dhahabu ya Miaka 50 ya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba)yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam,ambapo Mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais, Mhe,Balozi,Dkt.Emmanuel Nchimbi.


Waziri Kapinga amebainisha kuwa hatua hiyo itafungua masoko mapya,itaongeza thamani ya mauzo ya nje na kuinua uchumi wa wananchi kwa ujumla.


Mhe.Kapinga ameeleza kuwa,ili kujenga uchumi imara wa viwanda na wenye ushindani, kuna haja ya kubadili mtazamo wa kibiashara kwa kuhakikisha mazao ya kilimo,Mifugo,Uvuvi,Misitu na Madini yanageuzwa kuwa bidhaa zilizofungashwa vizuri na kukidhi viwango vya kimataifa. 


Waziri Kapinga, amesisitiza kuwa uwekezaji mkubwa katika teknolojia za kisasa una mchango mkubwa katika kuongeza kiwango cha uzalishaji,kuboresha ubora wa bidhaa zinazotengenezwa nchini,kupunguza gharama za uendeshaji na kuzipa bidhaa za Tanzania uwezo mkubwa wa kushindana katika soko la kimataifa.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu