Na Omary Mbaraka
Kusimamishwa kazi kwa watumishi hao, kunatokana na utekelezaji wa maelekezo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba aliyoyatoa wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya hivi karibuni katika Mkoa wa Tanga ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi.
Maelekezo yametolewa ya kusimamishwa kazi Watumishi wa umma 14 katika Halmashauri ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga kufuatia tuhuma za ubadhirifu wa fedha katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jengo la utawala la halmashauri hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Wilayani Muheza, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Mhe. Prof. Riziki Shemdoe wamesema Katika ziara aliyoifanya Waziri Mkuu mkoani Tanga, pamoja na shughuli nyingine, alitembelea na kukagua jengo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Muheza na kubaini uwepo wa changamoto katika utekelezaji wa mradi huo ambapo aliwaelekeza kuchukua hatua za haraka ili kubaini wahusika na kuchukua hatua stahiki.

0 Comments