Na Omary Mbaraka 

 Tarehe 23 Oktoba 2025 Chombo hiki Cha habari kiliandika habari zinazohusu hujuma kubwa za ukwepaji mkubwa wa Kodi zinazofanywa na wafanyabiashara maeneo ya kinyerezi na sinza  na kuahidi uchunguzi ukikamalika tutaweka bayana ili vyombo husika vichukue hatua

Hata hivyo Chombo hiki Cha habari kilipata tetesi kuwa mfanybiashara wa kinyerezi anaejulukana kwa jina moja Mwaseba anaendelea kuchukuliwa hatua na TRA hivyo basi mwandishi wa HABARI hizi Leo hii alikwenda kinyerezi kupata taarifa zaidi na kumkuta msaidizi wake ambae alikili kuwa suala la Kodi Bado linaendelea TRA na alimuomba Mwandishi huyo aongee na bosi wake bw Mwaseba kupitia simu yake (msaidizi) ilikuwa kati ya mida ya saa nne na dakika kumi na saa nne na dakika thelathini (4.10-4.30)

Mara tu Mwandishi alipopokea simu bw Mwaseba alimtamkia nanukuu "Wewe nitakupigia risasi" na Mwandishi huyo kubaki kushangaa huku akimuuliza ni kwa Nini  unipige risasi nimekosa Nini ?