Na Mwandishi wetu 

Usiku wa jumamosi tarehe 8 Novemba 2025 Mfanyabiashara na mkulima wa Kijiji Cha Nyambogo Ngerengere mkoani morogoro  bw Said Salum Mbaraka alivamiwa na watu wasiojulikana ambao walimpiga risasi mguuni na kumkata mapanga kichwani na mguuni na hivyo damu nyingi kumwagika na hatimae alifariki

Katika sakata Hilo majangili hao tv walifanikiwa kumchukulia mamilioni ya shilingi.

Kifo cha Mfanyabiashara huyo ambae alikuwa kipenzi Cha watu hapo kijijini,na hivyo kuwalazimu wanakijiji kuomba jeshi la polisi kufanya upelelezi yakinifu ili majangili hao wapatikane kwani kwa Hali ya Sasa watu wengi wamekuwa waoga  kujishughulisha na biashara ya mazao na kilimo