Na Mwandishi wetu
Afya za wafanyakazi katika kampuni hizi zipo mashakani kwani wanafanya kazi katika mazingira magumu ikiwemo maji machafu yanayotokana na kusafisha bidhaa ambazo ni uume wa ng'ombe
Kampuni hizi ambazo zinamilikiwa na raia wa china anaejulikana kwa jina la mama U na mwanawe Allan zinanunua na kusafirisha nchi za nje uume wa ng'ombe
Hata hivyo waandishi wa chombo hiki Cha habari walipotembelea eneo lao la kazi maeneo ya kiwalani maarufu" Kwa Guru"walielezwa kuwa wakurugenzi hawapo ambapo baadhi ya wafanyakazi walithibitisha kuwa wamefanya kazi kwa muda mrefu kati ya miaka miwili Hadi mitatu wakiwa ni vibarua jambo ambalo ni kinyume Cha sheria
Pia wafanyakazi hao walionekana wakiendelea na kazi katika Hali ya uchafu huku hawana vitendea kazi pia walikili kutembelewa na taasisi mbali mbali za serikali lakini mazingira ya kazi zao hayabadiliki Bado ni magumu



0 Comments