Blog Post

WAZIRI KIKWETE ASHIRIKI MAPOKEZI YA TUNZO YA RAIS DR SAMIA

 Na Omary Mbaraka 


Waziri wa kazi ajira na vijana wenye ulemavu ofisi ya waziri mkuu Mh Ridhwani Jakaya Kikwete ameshiriki mapokezi ya Tunzo ya Shukurani kwa Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada kubwa alizozifanya akiongoza mapambano kuwatetea na kuwahudumia Watu wenye Ulemavu , zilizopokelewa na Mh Kassim Majaliwa Majaliwa , Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa niaba yake Jana tarehe 11 Oktoba Dar- Es Salaam. 


Tunzo hii ambayo inabeba mrejesho wa shukrani kwa kazi nzuri ambayo Mheshimiwa Rais. Dkt Samia ameifanya kwa watu wenye Ulemavu katika kipindi cha miaka yake minne ya uongozi wake, ni alama ya shukrani toka kwa watu wenye Ulemavu. Kwa upande wake Mh Kikwete ametumia nafasi hiyo kumshukuru Mh. Rais kwa jinsi anavyo heshimisha kama nchi na hata leo matunda yake yanaonekana.


Naye Mh Majaliwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania amewashukuru watu wenye ulemavu kwa kutambua mchango huo kwa Mh. Rais na kuwapa salamu pia za Mh. Rais kuwa ataendelea kushirikiana nao.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu