Blog Post

MAMA WA KIHINDI ATAPELIWA NA MGANGA FEKI

 Na Mwandishi wetu 

Mama wa kihindi atapeliwa na mganga feki ajulikanae kwa majina ya Bandee au Mikidadi. 

Mwandishi wetu aliongea na mama huyo wa kihindi ajulikanae Kulsum Asgar Jaffer ambae alisema yeye ni mjane na akakili kuwa alikuwa akiwasiliana na mganga huyo amsaidie katika biashara zake ambazo zimepolomoka kwani hapo awali alikuwa na kantini yakulisha chakula shule ya Almuntazir na sasa amepata kantini katika shule ya Shaban Robert baadae ya kuondolewa Almuntazir 

Baada ya mganga huyo kuhojiwa alidai mama huyo bi Kulsum alimuomba awaue watu sita akiwemo viongozi wa shule ya Almuntazir hata hivyo hakuonyesha ushahidi wo wote mbali na meseji ambazo pia hazikuwa na agizo la kuua hata hivyo baada ya mganga huyo kujulishwa habari hizi zitachapishwa alituma meseji ya vitisho kwa Mwandishi wa habari hizi kuwa atamuua na atakufa kifo Cha Deo Mgasa

Pia Mwandishi wa habari hizi aliongea na Kulsum ambae alikili kuwasiliana na mganga huyo baada ya kutambulishwa katika simu na mlinzi mojawapo wa shule ya Shaban Robert ambae nae alikanusha hakumuagiza mganga huyo kuua ila alitaka viongozi hao wa Almuntazir waachishwe kazi


Post a Comment

0 Comments

Close Menu