Na Omary Mbaraka
Waziri wa kazi ajira na vijana wenye ulemavu ofisi ya waziri mkuu Mh Ridhwani Jakaya Kikwete tarehe 9 Oktoba alikwenda Mbeya kuangalia maandalizi ya sherehe za Kuhitimisha Mbio za Mwenge wa uhuru zitakazotanguliwa na Maonyesho ya kazi Mbalimbali na huduma katika Wiki ya Vijana na Kongamano kubwa litakalokutanisha vijana zaidi ya 1500, zinazotarajia kufanyika Mbeya mjini.
Maonyesho ya Wiki ya Vijana yalianza tarehe 8 Oktoba na kuhitimishwa tarehe 14 Oktoba 2025 pamoja na Kongamano la Vijana ambalo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mh Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania. Shughuli hizi zote zitahitimishwa na sherehe za kilele cha Mwenge wa Uhuru 2025 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Dr. Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika ziara hiyo Mh Kikwete alipata nafasi ya Kukagua matayarisho ya shughuli hizo zote na kukutana na wananchi, kuwasalimia na kuwakaribisha kuja kushiriki shughuli hizo zote.
"Karibuni sana Mbeya, tusikilize Nini mwenge wa Uhuru Umeona" alisema Mh Kikwete






0 Comments