Na Omary Mbaraka
Mh Ridhwani Jakaya Kikwete amefanya mkutano na Wananchi wa Kata ya Bwilingu katika Mji wa Mdaula, Msolwa na Chalinze ikiwa ni muendelezo wa kampeni kuomba ridhaa ya wananchi wakichague Chama Cha Mapinduzi ili kiweze kuongoza shughuli za maendeleo katika miaka Mitano inayokuja kuanzia mwaka 2025 hadi 2030.
Akizungumza na wananchi katika maeneo hayo aliwakumbusha mafanikio yaliyofikiwa katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi 2020-2025 na nia aliyonayo kiongozi wetu kuwa ndiyo msingi mkubwa unaotupa jeuri Chama Cha Mapinduzi. “… katika miaka minne iliyopita Rais Samia ametekeleza ilani kwa ufundi na weledi mkubwa ambapo unampa sifa ya kuwa jemedari bora katika mapambano ya ukombozi wa Watanzania katika nyanja zotr za kiuchumi, kijamii na pia mapambano dhidi ya maadui wakubwa wa nchi yetu.
Mh Kikwete aliwakumbusha pia tarehe 29 Oktoba ni siku muhimu kwa wana chalinze kwenda kumshukuru mgombea wa CCM kwa kukichagua chama hiki na wagombea wake kwa kupiga kura nyingi sana na kukipa ushindi mkubwa ili kiunde serikali kwenda kujibu kero au changamoto za wananchi.



0 Comments