Na Omary Mbaraka
Kwa mujibu wa sheria za Kazi zinazotoa mamlaka ya kutangaza Kima Cha Chini Cha Mshahara wa sekta binafsi, Jana Waziri wa kazi ajira na vijana wenye ulemavu ofisi ya waziri mkuu Mh Ridhwani Jakaya Kikwete ametangaza ongezeko la Kima Cha Chini Cha Mshahara kwa sekta binafsi kuwa kimeongezeka kwa asilimia 33•4 ambapo sasa kima Cha Chini kimeongezeka toka Shilingi 275,060 mwaka 2022 hadi Shilingi 358,322 mwaka 2025.
Zoezi hili ambalo ufanyika kila baada ya miaka mitatu, ni hatua nyengine kufuatia kukamilika kwa tamko la kima cha chini cha Mshahara kwa watumishi wa umma ambapo Serikali imepandisha mishahara kwa asilimia 35•1 ambapo sasa kima cha chini cha mishahara kuwa Shilingi 500,000 kama ilivyotangazwa na Dr. Samia Suluhu Hassan , Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania wakati wa kilele cha Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani. Hii ni alama nyengine ya mafanikio katika kuimarisha ustawi wa wafanyakazi Tanzania.




0 Comments