Na Mwandishi wetu
Chombo hiki Cha habari kimebaini ukiukwaji mkubwa wa Kodi unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wasio waadilifu wanaoagiza POMBE kadhaa kutoka Afrika ya kusini zikiwemo Savannah, Brutal Henkel nk
Baada ya kutumia mbinu kadhaa kuzivusha mipakani huzifikisha katika maghala yao na kufanya ukarabati wa kubandika stika za TRA feki ama walizopata kwa mbinu chafu na kuziingiza sokoni
Chombo hiki Cha habari kikikamilisha uchunguzi kitafichua mbinu hizo haramu ambazo zinakosesha Taifa mapato yake Baada ya chanzo chetu Cha habari kutuonyesha maeneo mawili ya watuhumiwa hao katika maeneo ya Sinza na Kinyerezi,
Ingawaje pia vyanzo vyetu vya habari vimebainisha kuwa mmoja anaetuhumiwa baada ya kuelezwa ujio wetu na kumkosa amejipanga kutumia vibaya jeshi la polisi ili kudhoofisha juhudi ya chombo chetu Cha habari kufichua hujuma hizo jambo ambalo pia ni kwenda kinyume na katiba yetu ya nchi ya mwaka 1977 ibara ya 18



0 Comments