Blog Post

WAZIRI KIKWETE ALITOA TAARIFA YA MAANDALIZI KABLA YA MEI MOSI

 





Na Omary Mbaraka 

Waziri wa kazi ajira vijana na wenye ulemavu ofisi ya waziri mkuu Mhe Ridhwani Jaksya Kikwete alitoa taarifa ya ukamilifu na Utayari wa maandalizi ya kilele cha Sherehe za Mei Mosi zilizofanyika leo  tarehe 1 Mei, kayika viwanja vya Bombadier, Manispaa ya Singida kwa Mh. @kassim_m_majaliwa , Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania . Akizungumza baada ya ukaguzi na kupokea taarifa, Waziri Mkuu wa JMT ameeleza kuridhishwa na maandalizi na kupongeza maandalizi yaliyofanyika ambapo ameeleza kuwa na viwango vikubwa sana kuliko kupata kutokea.

Pia Mhe Kikwete  alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi na wafanyakazi wote  kusherehekea mafanikio ya miaka minne ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu