Na Mwandishi wetu
Meli mbili ziligongana katika bandari ya Dar es salaam moja iliotoka ufaransa ikijulikana kwa jina la MV GRECO LIBERO ambayo ilikuwa imebeba TANI 6138 za mbolea iliokuwa zikienda zambia ambazo zote ziliharibika baada ya kumwagiwa na mafuta
Baada ya kulipwa na bima, kampuni ambayo ni wakala wa meli hio Express Chartering & Shipping Ltd ikishirikiana na kampuni ya Inchcape Shipping agency ambayo iliiteua kampuni ya MSTJ Traders T Ltd kusomba mbolea hio na kwenda kuifukia chini ya ardhi.Pia kampuni ya Express Chartering Shipping agency iliziandikia taasisi zote husika za SERIKALI ikiwa pia ilizionya kampuni zote zitakazoshitiki zoezi kufanya shughuli hio kwa nidhamu wasitoe rushwa wala wasidhulumu watendaji
Hivyo basi baada ya MSTJ Traders kupokea fedha za kimarekani Dola milioni 1.4 na kusani mkataba na kampuni ya Mohaza Shipping ili itoe wataalamu wake kusomba mbolea hio na kwenda kuizika palizuka malumbano makubwa ya makampuni kadhaa kwani kampuni ya ya Mohaza Shipping pamoja na kupata mkataba huo ilijikuta imetelekezwa kwani MSTJ Traders iliiteua kampuni nyingine ijulikanayo Chillambo General yenye masikani yake Kisarawe mkoani Pwani, ambapo pia Kuna mtu ajulikanae Hidaya nae alipewa jukumu la kutafuta malori ili yabebe mbolea hio na kuipeleka Kisarawe ambapo ndio mbolea hio ilizikwa
Utata mwngine uliojjitokeza baada ya zoezi Hilo kufanyika kikamilifu kampuni ya Chillambo General imesema Bado inaidai kampuni ya MSTJ Traders T shilingi milioni 154 vile vile haijulikani ni kwa Nini kampuni ya MSTJ Traders ilihamisha fedha dola za kimarekani laki 462 kutoka katika akaunti yake iliopo CRDB Tawi la Temeke kwenda kwa mfanyabiashara mmoja mwenye asili ya kihindi ambae hakuwemo katika zoezi Hilo na ni kinyume na Sheria za SERIKALI
Isitoshe utata mwingine ulijitokeza kwa vile NEMC ilipaswa kulipwa shs milioni 14 ili iwafundishe madereva wa malori yapatao 70 jinsi ya kubeba mzigo wa mbolea iliyoharibika ambapo kwa kila dereva alipaswa kulipiwa shs laki tatu na hamsini (350000) na hivyo serikali imekosa kipato hicho
0 Comments