Na Omary Mbaraka
Waziri wa kazi ajira vijana na wenye ulemavu ofisi ya waziri mkuu Mhe Ridhwani Jakaya Kikwete akiongea mbele ya umma wa Wafanyakazi waliojaa kwenye uwanja wa Bombadier , katika manispaa ya Singida alimshukuru Mh. Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kwa miongozo yake na mazingira aliyoyawezesha kwa Watumishi wa Tanzania katika miaka Minne ya Uongozi wa Nchi yetu.
Mhe Kikwete aliendelea kumshukuru Mh. Rais kwa kuongeza mishahara kwa Asilimia 35. Haya ni mafanikio makubwa na ameonyesha uongozi mkubwa sana. Kwa hakika Utu na Kazi sio Msemo wa Kisiasa Bali ni maisha yako na tunakushukuru sana. Alisema Mhe Kikwete
0 Comments