Blog Post

WAZIRI KIKWETE ATEMBELEA MAANDALIZI YA MEI MOSI SINGIDA






Mapema leo, Waziri wa kazi,ajira,vijana na wenye ulemavu ofisi ya waziri mkuu Mhe Ridhwani Jakaya Kikwete ametembelea Manispaa ya Singida, kuangalia maandalizi ya sherehe za Sikukuu ya Wafanyakazi ( Mei Mosi). Ambapo amekuta Maandalizi yanakwenda vizuri na hatua iliyopo sasa ni zaidi ya Asilimia 88. 

Aliwashukuru sana Viongozi wa TUCTA wakiongozwa na Katibu Mkuu Ndg. Henry Mkunda kwa kazi nzuri akishirikiana na uongozi wa Mkoa chini ya Cde. Halima Dendegu. 

Mei Mosi hii inakwenda peleka Neema na mabadiliko makubwa Mkoa wa Singida. 

Post a Comment

0 Comments

Close Menu