Na Ismail Mang'ola, Dar
Wananchi wa mtaa wa Chang'ombe 'A' wakihakiki majina yao katika orodha ya majina kabla ya kwenda kwenye sanduku la kupigia kura.
Muonekano wa wapiga kura katika vituo vya kupigia kura kwa ajili ya kuwapata viongozi wa Serikali za mitaa Mwenyekiti na wajumbe wake watano umefanyika kwa utulivu mkubwa
Katika maeneo mengi ambayo Tafakari News Weblog imetembelea imekuta Hali ya utulivu wa Hali ya juu licha ya wpiga kura kutoonekana kwa wingi Kama ilivyozoeleka kwenye uchaguzi mkubwa.
Kituo Cha mtaa wa Chang'ombe 'B' Hali ya utulivu ilionekana kushika nafasi yake lakini pia hata kituo Cha Chang'ombe 'A' kimeonekana kuwa na utulivu sambamba na wananchi kuonyesha Hari ya upendo katika kuhakikisha wanapata haki yao ya kumchagua kiongozi wanayemtaka.
Katika mtaa wa Kata 14 Temeke Hali ya wapiga kura haikutofautiana na maeneo mengine ambayo Tafakari limefanya mizunguko yake lakini mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, alionekana kulalamika akidai Hana Imani na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakihitaji maelekezo.
Kwa upande wa Mtaa wa Toroli ambapo mgombea wake ndio msimu wake wa kwanza kukiomba kiti Cha nafasi ya Mwenyekiti Omari Hashim Kifundo (Nyuki) pia Hali ya utulivu imeonekana kupata nafasi kubwa na kuwafnya wanausalama kujipatia nafasi ya kupumzika bila ya mvutano wa hapa na pale Kama ilivyozoeleka.
Mkazi wa Chang'ombe 'A' akipiga kura kumchagua kiongozi anayemtaka Kama alivyokuwa akionekana na kamera yetu maeneo ya Chang'ombe 'A' Temeke jijini Dar es Salaam.
0 Comments