Blog Post

VUTA NIKUVUTE YAIBUKA MSIBA WA DIDA BAADA YA MAJIRANI KUTORIDHIKA

 Na Omary Mbaraka

Mamia ya majirani na ndugu wa karibu wa marehemu Khadija Shaibu maarufu Dida waliibuka na kudai ratiba ya MAZISHI haikuwatendea haki.

Hayo yalisikika mbele ya Mwandishi wetu nyumbani alikozaliwa marehemu Dida maeneo ya shekilango ubungo. Mzee mmoja wapo jirani bw James Nyanda alisema"Hakika hii ratiba ya mazishi haikutendea haki wakazi wa hapa ambapo wengine walimuona Toka akizaliwa na mabinti wengine walikua pamoja nyakati za utotoni mpaka ukubwani walitegemea maiti ingetoka hospitalini na kuja nyumbani ambapo heshima za mwisho zingefanyika na baadae kupelekwa msikitini na mwishowe makaburini."

Hakika umati mkubwa uliokusanyika wakiwemo ndugu wa karibu walisikitishwa sana na baadhi yao wakidai "Hatukufuata Kula wali hapa kwani hata kwetu upo tulikuja kumpa heshima za mwisho marehemu na tunaamini hata yeye huko alipo hakuridhika na hii yote ni wakubwa wameharibu ratiba

Hivyo basi Mwandishi wetu alishuhudia malalamiko mengi tu kutoka pia kwa akina dada waliokuwepo wakidai kwa sauti kubwa ya kukasirika "Tunamuhitaji Dida hapa, Dida kazaliwa hapa na kakulia hapa katika nyumba hii ambapo pia mama yake mzazi alifia hapa"zilisikika sauti kadhaa kwa ukali.

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania pia ametoa salam za rambi rambi kwa familia ya marehemu na kwa waganyakazi wa wasafi media group 


Post a Comment

0 Comments

Close Menu