Na Omary Mbaraka
Waziri wa kazi, ajira na vijana wenye ulemavu Mhe Ridhwani J Kikwete Akutana na makundi mbalimbali kuhamasisha maandalizi ya shamra za kuadhimisha kilele Cha mbio za mwenge
Huku akiwatembelea Vijana wa Haraiki.
Mh. Kikwete amefanya ziara ya siku mbili mkoani Mwanza ikiwa ni kukagua maandalizi ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru zinazotaraji kuhitimishwa mkoani hapo Oktoba, 14 mwak huu kwenye uwanja wa CCM kirumba.
Akiwa mjini Mwanza ,Waziri Kikwete amepata nafasi ya kukutana na makundi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha ushiriki wa kilele hicho na wiki ya Vijana ambayo inataraji kuanza tarehe 8 hadi 13 Oktoba 2024 katika viwanja vya furahisha.
Waziri Kikwete ambaye alikuwatana na makundi ya Vijana Wasanii katika fani mbalimbali na baadae kukutana na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Walimu wa sekondari na vyuo toka wilaya zote za Mkoa huo, alitumia nafasi hiyo kuwahimiza kujitokeza kwa wingi na kuhakikisha kuwa wanaulaki Mwenge kwa shamra nyingi na kushiriki kilele cha wiki ya vijana.
Baada ya mikutano hiyo ya Wadau , Waziri Kikwete alifika Uwanja wa CCM Kirumba kuona maandalizi ya haraiki ambapo alishuhudia vijana wakiendelea na maandalizi yao na katika salamu zake aliwapongeza walimu wa vijana hao na kuwatia moyo wanafunzi ambao wameandaliwa vizuri. Uwanjani hapo
0 Comments