Blog Post

MAMA AONYA UAPISHWAJI MAWAZIRI LEO


Na MWANDISHI WETU

Rais Dk Samia Suluhu Hassan amewaonywa Viongozi wote walio pewa dhamana kukumbuka kuwa cheo ni sawa na nguo ya kuazima hivyo wanapaswa kutenda kazi kwa uadilifu na kwa masilahi ya nchi, ameyasema hayo wakati akiwaapisha viongozi walio teuliwa hivi karibuni baada ya utenguzi.

Acheni kutanguliza matamanio yenu mkasahau wajibu wenu kama viongozi.

Amewaonya viongozi wote kujirekebisha kabla hajagundua nyenendo zao maana panga litawashukia bila kuwaangalia usoni.

Aidha, kwa upande wake Makamu wa Rais Dkt. Mpango amewatahadharisha viongozi wote kuwa; wasijidanganye kuwa nafasi zao haziwezi kuzibika na kujifanyie wanavyotaka wataadhirika.

Tupo pamoja na Rais wetu kwa kila jambo analolifanya kwa masilahi ya wananchi na Taifa letu.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu