Na Omar Mbarak
Tamasha la michezo la kila mwaka la shule za Sunrize lililofanyika leo kwenye viwanja Leaders Club Kinondoni, jijini Dar es Salaam, limewavutia watu wengi waliohudhulia tamasha hilo.
Katika tamasha hilo lililoanza asubuhi ya leo kwa kufanyika michezo ya aina mbalimbali.
Katika mchezo wa mpira miguu , mchezaji wa mpira wa miguu shule za Sunrise, Simon Bishanga amekuwa kivutio kikubwa katika tamasha la michezo ya kila mwaka lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Simoni kijana mdogo kutoka katika kundi la Gold alionekana kuwa nyota wa michezo hiyo baada ya kunesha mchezo mzuri na kubahatika kufunga goli katika mchezo.
![]() |
Wazazi wakiwa na wanafunzi kwenye tamasha la michezo la kila mwaka la shule za Sunrise lilifanyika leo viwanja vya Leaders Club |
Katika tamasha hilo wanafunzi waligawanywa katika makundi mbalimbali ili kushiriki michezo kwenye tamasha hilo ikiwa ni pamoja na kundi la Gold, Silver, Platinum nk
Tamasha hilo lilihudhuliwa na watu mbalimbali wakiwemo wazazi ambalo hakika matokeo yake ni kujenga afya za watoto na kudumisha mahusiano mazuri kati ya wanafunzi, wazazi na viongozi wao.
Katika mchezo wa riadha ambayo ilifanya kwa makundi tofauti, moja wa mbio hizo mjukuu wa aliyekuwa waziri mstaafu Maua Daftari alishinda mbio hizo.
Katika tamasha hilo ilifanyika michezo mbalimbali kama vile kuruka kamba, kucheza, kupuliza maputo, mbio za magunia, kuvuta kamba na mingine mingi.
0 Comments