Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, amerejea Zanzibar akitokea Dodoma aliposhiriki kikao Maalum cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC).
Pia, ameshuhudia hafla ya utiaji saini mikataba mitatu ya uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam kati ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kampuni ya DP World ya Dubai iliyofanyika Ikulu, Chamwino leo tarehe 22 Oktoba 2023.
Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Idrissa Kitwana na Viongozi wengine wa Chama na Serikali pamoja na vikosi ya Ulinzi na Usalama vya SMZ na SMT.
22 Oktoba 2023
Zanzibar.
0 Comments