Blog Post

NIDHAMU YAMPA MANDONGA UBALOZI MR DISCOUNT SUPERMARKET

 


Mkurugenzi wa Kampuni ya Mr Discount Hyper and Supermarket Ltd, akimkabidhi bondia wa ngumi za kulipwa nchini Bw. Karim Mandonga viatu vya Relaxo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam wakati akitangazwa kuwa balozi wa kampuni hiyo.


Na IBRAHIM KADILO

Mkurugenzi wa kampuni ya Mr Discount Hyper and Supermarket, imemtangaza bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Karim Mandonga kuwa balozi wa kampuni hiyo.

Mkurugenzi wa Makampuni ya Mr Discount Hyper Supermarket Ltd na Best Brand Distributor, Bw Khalid Mbarak Salim, akizungumza na waandishi wa habari Mlimani City jijini Dar es Salaam, alisema wamemtangaza Mandonga kuwa balozi rasmi wa kampuni hizo kutokana na nidhamu yake katika mchezo wa masumbwi.

Bw. Khalid alisema kuwa mkataba wa udhamini wa kuitangaza kampuni hizo na viatu vya Relaxo na Mandonga ni wa kutosha na utaendelea kulingana na nidhamu yake na ufanisi wake katika mchezo wa masumbwi.

"Tusingependa kuweka wazi  mkataba wake, huu ni wa kutosha na  tunafikiria pia kudhamini mchezo wa soka", alisema Bw. Khalid.

Bw. Khalid alisema kuwa wamelenga kuunga mkono michezo nchini kwa kuanza na mchezo wa masumbwi na kuwataka wananchi kujitokeza kutoa maoni yao kupitia akaunti zao za kijamii kupendekeza mchezaji wa soka atakayepata udhamini wa kampuni hizo hivi punde.

Alisema kuwa Mandonga atakuwa akipata ufadhili wa vifaa vya michezo na itamsaidia kujulikana ndani na nje ya nchi kwa kuwa viatu vya Relaxo vinazalishwa nchini India ambapo Mandonga ataanza kujulikana zaidi huko kama balozi wa viatu vya Relaxo.

Akaongeza kuwa kampuni zake ni za kizalendo na kuwataka makampuni mengine kujitokeza kuunga mkono wanamichezo wa hapa nchini.

Akizungumza kwa upande wake Mandonga alishukuru uongozi wa kampuni hizo kumtangaza kama balozi wao, na kuahidi kuitangaza kampuni hiyo kwa moyo na kudumisha nidhamu katika mchezo huo wa masumbwi.


Mkurugenzi wa Kampuni ya Mr Discount Hyper and Supermarket Ltd, Bw. Khalid Mbarak Salim akimpongeza bondia wa ngumi za kulipwa nchini Bw. Karim Mandonga kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam wakati akitangazwa kuwa balozi wa kampuni hiyo.

Post a Comment

0 Comments

Close Menu