Hayo yamesemwa Augosti 8,2023 mara baada ya Kamati hiyo kufanya ziara ya
kutembelea Miradi mbalimbali katika Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam, DUCE
ambapo wamepongeza juhudi ambazo zinafanywa na Chuo hicho.
Akizungumza
katika ziara hiyo Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Elimu,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Husna Sekiboko amesema kuna umuhimu mkubwa
Wizara kuhakikisha inatoa fedha kwaajili ya kukamilisha miradi hiyo kwani Chuo
Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, (DUCE) kimeanzisha miradi hiyo hivyo
inatakiwa wapewe ushirikiano kukamilisha miradi hiyo.
Amesema miradi inakwenda
vizuri na ubora wa ujenzi uko vizuri na inaonekana uhitaji ni mkubwa katika
matumizi ya miradi hiyo itakapokamilika.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia, Mhe.Omary Kipanga amesema wamepokea maagizo kutoka kwa
Kamati, hivyo Wizara itatekeleza maagizo hayo ili kuhakikisha miradi ambayo
inasimamiwa na DUCE inakamilika kwa muda ambao umewekwa ili kuhakikisha
utekelezaji wa majukumu kwenye maeneo hayo.
"Wizara tutakuja kuongeza fedha ili
miradi iweze kukamilika ndani ya miezi minne kama maagizo yalivyotolewa ili
ifikapo mwezi Januari wanafunzi wetu waweze kuyatumia kikamilifu". Amesema Mhe.
Kipanga
Pamoja na hayo Naibu Waziri Kipanga ameipongeza Menejimenti ya Chuo kwa
kuibua majengo hayo na kuona umuhimu wa kukamilisha miradi hiyo ambayo itakuwa
na msaada mkubwa itakapokamilika.
Naye Mkuu waChuo Kikuu Kishiriki Cha Elimu
(DUCE), Prof. Stephen Maluka amesema kwenye jengo la shule ya msingi wametumia
takribani shilingi milioni 350 na ujenzi unatarajia kukamilika mwezi Novemba
2023 kwa madarasa manne na ofisi, na kwa upande wa jengo la maabara mpaka sasa
wameshatumia Shilingi milioni 553 na ujenzi bado unaendelea.
0 Comments