
Na Mwandishi Wetu
KIJANA mmoja anayefahamika kama Miraji Salum mkazi wa Mbagala amepoteza mkono wake wa kulia baada ya kukatwa na mashine kazini kwake.
Chanzo chetu kimesema kwamba Miraji amepoteza mkono huo baada ya kukatwa na mashine ya kusagia plastiki kazini kwake katika kiwanda cha Zain Plastic kilichoko mtaa wa Makuka kata ya Mbagala Kuu jijini Dar es Salaam, Julai 26 mwaka huu.
Mmoja wa maofisa wa Kiwanda hicho aliyejitambulisha kwa jina la Feisal amekiri kutokea tukio hilo akisema kwamba Miraji alipatwa na janga hilo wakati anasafisha mashine ya kuchakata plastiki hizo.
Amesema kwamba kiongozi wa kazi wa idara hiyo ndiye aliyemwambia Miraji arudie kusafisha mashine hiyo, na wakati anasafisha kwa bahati mbaya mfanyakazi mwenzake alibonyeza kitufe cha kuwashia mashine hali ambayo ilimfanya Miraji kukatwa mkono huo.
Feisal amesema kwamba wako kwenye mazungumzo na familia yake kuangalia jinsi wanavyoweza kumtibia, na mfanyakazi huyo amelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Temeke kwa matibabu.
Tukio hilo limegubikwa na utata mkubwa, na Ripoti Kamili tutaileta katika Ripoti kamili ambayo tutaichapisha katika mtandao huu, pamoja na taarifa za wadau wengine.
0 Comments