Na Mwandishi wetu
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Judith Kapinga amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa biashara ya kimataifa wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Mhe Julien Paluku Kahongya na ujumbe wake uliopo nchini kwa ziara ya kiserikali
Mhe Kapinga amesema kuwa Tanzania na Congo Ina ushirikiano wa muda mrefu kwenye sekta za usafirishaji, miundombinu ya usafirishaji hususani kwenye bandari ya Dar es salaam na kuongeza kuwa Tanzania Ina nafasi kubwa ya ushirikiano Kati yake na Congo
Aidha Mhe Kapinga Ameongeza kuwa kwa sasa Tanzania imejipanga kuhakikisha inakuza sekta ya Viwanda na biashara ili kufikia uchumi wa Dola trilioni moja ifikapo 2050 na kuhakikisha nchi inauza zaidi bidhaa zilizoongezwa thamani badala ya kuuza malighafi pekee.
Kwa upande wake Waziri wa Biashara wa Congo Mhe Julien Paluku Kahongya amesema kuwa Congo inanufaika sana na uwepo wa bandari ya Dar es salaam kwa kuwa asilimia kuwa ya bidhaa za Congo zinapitia bandari ya Dar es salaam hivyo mahusiano ya kibiashara Kati ya Tanzania na Congo ni ya muhimu sana.
Ujumbe wa Waziri wa Congo uliambatana na Balozi wa Congo hapa nchini na wawakilishi kutoka serikalini ambapo ziara yao ni mwendelezo wa ziara aliyoifanya Rais wa Congo kutembelea hapa nchini mwezi wa nane mwaka huu.






0 Comments