Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Albert Chalamila ametembelea maonesho ya 50 kimataifa ya biashara Dar es salaam Sabasaba na kuwahimiza wananchi kuendelea kutembelea Maonesho hayo ili kujipatia huduma na bidhaa mbalimbali akisema maonesho hayo yanatoa fursa ya kujifunza teknolojia mpya, kupata huduma za Serikali na sekta binafsi pamoja na kununua bidhaa kwa bei nafuu huku akieleza nia ya kuongeza muda wa maonesho hayo.
Akizungumza katika viwanja vya maonesho hayo ya 50 ya kimataifa ya biashara Dar ee Salaam RC Chalamila amesema kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi, Mkoa unatafakari uwezekano wa kuongeza siku za maonesho ili watu wengi zaidi wanufaike huku akitoa wito lwa wananchi kuendelea kujitokeza.
RC Chalamila amesema maonesho hayo yakiwa yamefikisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake mwaka huu kuna mataifa yapatayo 25 ambayo yameshiriki hivyo ni muhimu kwa wananchi kuyatumia kama fursa ya kupata bidhaa na huduma mbalimbali ambapo amesisitiza kuwa bidhaa nyingi zinapatikana kwa bei ya punguzo.
Aidha Chalamila amezungumzia huduma za matibabu ya macho zimazopatikana viwanjani hapo bila malipo pamoja na huduma mbalimbali za kisheria ikiwemo kwenye masuala ya ardhi hivyo amewataka wananchi kuyatumia maonesho hayo kama fursa adhimu
Kwa upande wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Muliro Jumanne, amesema hali ya usalama katika jiji hilo ni shwari, huku wananchi wakiendelea kujitokeza kwa wingi kutembelea maonesho hivyo mesema vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kufanya kazi kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao unaimarika katika kipindi chote cha maonesho.
Baadhi ya wananchi waliotembelea maonesho hayo wamesema Sabasaba ya mwaka huu imekuwa na maboresho makubwa, ikiwemo ongezeko la huduma za Serikali, bidhaa mbalimbali kwa bei za maonesho pamoja na huduma za afya, elimu na ushauri zinazowawezesha kutatua changamoto mbalimbali katika eneo moja.



0 Comments